Maneno 24 Ya Ushawishi Yenye Nguvu Ya Kukupa Chochote Unachotaka.
Rafiki yangu mpendwa,
Ili upate kile unachotaka kwenye maisha yako, lazima kwanza uwape wengine kile wanachotaka.
Utaweza kuwapa wengine kile wanachotaka kama utakuwa na ushawishi mkubwa kwao na kuwafanya wakuamini.
Njia bora ya kuwafanya wengine washawishike na wewe ni kujua jinsi saikolojia ya binadamu inavyofanya kazi na kuweza kuitumia kwa usahihi.
Sisi binadamu huwa kuna maneno tukiyasikia tunaamini na kushawishika haraka sana. Maneno hayo yanagusa mazoea ambayo tunayo na kutulazimisha kufanya vitu bila ya kuona tunalazimishwa.
Hayo ndiyo maneno ya ushawishi ambayo mtu ukiyajua na kuyatumia unakuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine na kuweza kupata chochote unachotaka.
Kuna maneno 24 ya ushawishi ambayo ukiyajua na kuyatumia vizuri, unakuwa na ushawishi mkubwa kwa wengine. Orodha ya maneno hayo ni kama ifuatavyo;
1. Sina Uhakika Kama Itakufaa, Lakini….
2. Mtazamo Chanya.
3. Unajua Nini Kuhusu.…?
4. Utajisikiaje Kama….?
5. Pata Picha….
6. Upi Utakuwa Muda Mzuri Kwako?
7. Nadhani Bado Hujaweza….
8. Kugeuza Swali.
9. Una Machaguo Matatu.
10. Aina Mbili Za Watu.
11. Naamini Upo Kama Mimi.
12. Ikiwa……Basi……
13. Usiwe Na Wasiwasi.
14. Watu Wengi….
15. Habari Njema.
16. Kinachofuata Baada Ya Hapa.
17. Nini Kinakufanya Useme Hivyo?
18. Kabla Hujafanya Maamuzi….
19. Kama Niki… Je Wewe Uta…?
20. Je ... Inakutosha?
21. Kitu Kimoja Zaidi.
22. Msaada.
23. Ningependa Tu Kujua….
24. Kinafanya Kazi Vizuri Sana.
Ufafanuzi wa jinsi maneno hayo yanafanya kazi na kuwa na ushawishi mkubwa kwa mtu uko hapo chini kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA. Fungua kipindi hicho ili ujifunze na kuweza kutumia maneno ya ushawishi kwa usahihi na manufaa.
kwenye kitabu cha CHUO CHA MAUZO, Moduli ya sita imebeba maneno hayo ya ushawishi, yakiwa yameelezewa kwa kina na mifano halisi ya jinsi yanavyoweza kutumika kwa manufaa.
Hakikisha una nakala yako ya kitabu cha CHUO CHA MAUZO ambacho kinakujenga wewe kuwa muuzaji bora na kufanya mauzo makubwa. Wasiliana sasa na namba 0678 977 007 kupata nakala yako ya kitabu.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.