Ubongo wetu binadamu ni kiungo chenye uwezo mkubwa sana. Japo kinachukua asilimia 2 tu ya mwili mzima, ndiyo kinachochukua nguvu nyingi kwenye chakula ambacho tunakula. Binadamu ndiyo viumbe pekee ambao wana ubongo ulioendelezwa na wenye uwezo wa kufikiri na kufanya maamuzi mbalimbali.
Lakini kama ulivyo usemi maarufu, madaraka makubwa yanakuja na uwajibikaji mkubwa. Uwezo mkubwa wa ubongo na akili tulionao, unahitaji kudhibitiwa vizuri sana kama tunataka kuweza kutumia uwezo huo kufanya makubwa. Hiyo ni kwa sababu akili ikiachwa tu ijiendee yenyewe, huwa inajisumbua na kujipoteza, kitu kinachoifanya ikose ufanisi.
Akili yetu inayofikiri huwa inafananishwa na nyani ambaye hawezi kutulia kwenye tawi moja la mti. Kila mara nyani huwa anaruka kutoka tawi moja kwenda tawi jingine. Hivyo pia ndivyo akili zetu zilivyo, huwa haziwezi kukaa na wazo moja kwa muda mrefu. Bali akili huwa inaruka ruka kutoka wazo moja kwenda wazo jingine.
Huwezi kufanya makubwa kama akili yako inaruka ruka kutoka wazo moja kwenda wazo jingine. Ili uweze kufanya makubwa unapaswa kutuliza mawazo yako kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu zaidi. Umakini na kuzingatia ni vitu vinavyohitajika sana kwa mtu kuweza kufanya makubwa. Lakini pia siyo vitu rahisi kufanya, hasa ukizingatia asili ya akili kuruka ruka.
Zipo njia mbalimbali za kuituliza akili, ili uweze kuweka umakini na uzingativu wako kwenye kitu kimoja kwa muda mrefu. Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeeleza kwa kina kwa nini akili zetu zipo hivyo zilivyo na njia za kutuliza akili ili kuweza kufanya makubwa. Ni njia ambazo kila mtu anaweza kuzitumia kwa uhakika na kupata mafanikio makubwa.
Karibu usikilize kipindi hicho cha ONGEA NA KOCHA hapo chini, uende ukafanyia kazi hizo njia za kutuliza akili na uweze kufanya makubwa kwenye maisha yako.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.
Nakala nzuri sana yenye mafunzo mazuri ahsante sana