🔥*Huyu Ndiye Mjasiriamali Asiye Wakawaida!* 🔥
Kakaa/Dadaa Yangu,
💥 Unajua shida ya wengi?
Wengi wanaanza biashara kwa kishindo...
Lakini baada ya miezi mitatu,
BAM! Kimya kama kaburi la usiku.
Wanaanza kuuza nguo,
Wanaingiza mzigo wa milioni mbili,
Lakini hakuna anayenunua.
Wanashindwa kuelewa nini kinakwenda kombo.
Wanakata tamaa fasta.
Wanarejea kutegemea mshahara.
Wengine wanakata tamaa kabisa—wanakufa na ndoto zao.
💔 Na hapa ndipo kuna maumivu makali.
Biashara si kupost tu bidhaa kwenye status.
Si kutegemea rafiki zako watanunua.
Wala si kushusha bei kila siku eti "promo."
Ukiwa huna akili ya mjasiriamali mjanja
utachezewa kama karata mitaani.
🎯 Ngoja nikufunze kitu.
Mjasiriamali mjanja ana akili ya pesa.
Anajua kutafuta wateja wake popote.
Anajua jinsi ya kuwashawishi bila kusumbua.
Anajua kutoa ofa ambayo haiwezi kukataliwa.
Anaelewa psychology ya mteja.
Na zaidi ya yote, anajua kuji-brand.
Na kama hujui hayo yote,
Usijidanganye eti “ni mapenzi ya Mungu.”
Ni mapenzi ya kukosa maarifa.
⚙️ Sasa suluhisho liko hivi:
Ukiamua kuwa mjanja kwenye biashara
Lazima ujue kuuza hadithi.
Ndiyo, HADITHI!
Watu wananunua stori kabla ya bidhaa.
Wakiigusa hadithi yako,
Wanafika mwisho wa status tayari wamejishawishi.
Ukiuza sabuni,
Usiuze sabuni uza usafi wa mtoto wao.
Ukiuza viatu,
Usiuze kiatu uza heshima ya mguu wake kazini.
Mjasiriamali mjanja anauza HISIA si bidhaa tu.
🧠 Nikupe hadithi moja ya kweli.
Mrembo mmoja anaitwa Amina.
Alikuwa anauza mikoba Kariakoo.
Alihangaika sana, kila siku status 50, likes 2, wateja 0.
Alipojifunza kuuza kwa stori, mambo yalianza kubadilika.
Siku moja aliandika:
“Mwanamke mmoja alikuja dukani kwangu, akiwa amechoka, alinyamaza muda mrefu...
Aliponunua hii handbag,
Alisema, ‘Kwa mara ya kwanza najihisi mwanamke kamili.’
Niliogopa kusema chochote,
Ila moyo wangu ulichanua.
Na hapo ndipo nilijua,
Siuzi mikoba, nauza imani kwa mwanamke.”
Dakika 20 baadaye mikoba 7 iliuzwa.
🔥 Sasa uliza tena… MJASIRIAMALI MJANJA ni nani?
Ni yule anayejifunza kila siku.
Anayefikiria tofauti.
Anayejua kutumia lugha ya wateja.
Anayeuza kwa hisia, si bei.
Wewe je?
Upo kwenye biashara kwa bahati,
Au umeamua kuwa MJASIRIAMALI MJANJA?
😎 Kumbuka hii ya mwisho:
Wakati wengine wanauza bidhaa,
MJANJA ANAUZA STORI INAYOCHOMA MOYO.
MUHIMU; Kama bado hujasoma kitabu cha MJASIRIAMALI MJANJA,
Ukweli ni kwamba unajipunja,
Kukipata Piga Simu 0756694090.
Karibu.
Rafiki Yako Anayekupenda Na Kukujali Sana,
Mkufunzi Ramadhan Amir.