Biashara Ni Vita Kali Na Hivi Ndivyo Unavyoweza Kuishinda Kwa Uhakika.
Kwa zama tunazoishi sasa, biashara ndiyo njia ya kutengeneza kipato kikubwa na cha uhakika kwa mtu yeyote yule. Hiyo ni kwa sababu ajira zimekuwa chache, wakati watu bado wana mahitaji. Hivyo yeyote anayeweza kutatua mahitaji ambayo watu wanayo, anaweza kujihakikishia kuwa na kipato.
Pamoja na uhakika huo wa biashara kwenye kipato, bado siyo kitu rahisi kufanya na kufanikiwa. Tafiti zinaonyesha biashara nyingi mpya huwa hazivuki miezi sita ya kwanza, na hata zinazovuka hiyo miezi sita, nyingi zaidi hazivuki miaka miwili.
Biashara ni ngumu kwa sababu soko ni sawa na uwanja wa vita, vita ambayo ni ngumu na maadui hawana huruma. Na kibaya zaidi, maadui ambao mtu unakuwa unapambana nao kwenye biashara ni wengi na unakuwa huwajui moja kwa moja.
Wengi wanaposikia kuhusu maadui wa biashara huwa wanafikiria ni washindani. Lakini washindani ni adui wa tatu, tena ambaye madhara yake siyo makubwa kama ya adui wa kwanza na wa pili.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA nimeshirikisha maadui wakuu watatu kwenye vita ya kibiashara na jinsi ya kuwashinda ili uweze kufanikiwa. Usianze au kuendelea kujenga biashara yako kama bado hujawajua maadui hawa watatu. Kwani madhara yao, hasa wawili ambao hawaonekani moja kwa moja ni makubwa.
Karibu usikilize kipindi hicho cha ONGEA NA KOCHA, ujifunze na kwenda kufanyia kazi ili kujenga na kukuza biashara yenye mafanikio makubwa. Kipindi kipo hapo chini.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
0678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 2. KISIMA CHA MAARIFA, 3. CHUO CHA MAUZO na 4. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.