BIASHARA NDANI YA AJIRA; Mwongozo Wa Kuanzisha Na Kukuza Biashara Yako Ukiwa Kwenye Ajira.
BIASHARA NDANI YA AJIRA ni kitabu ambacho kinakupa maarifa, mikakati na mbinu za kuanzisha na kukuza biashara yako ukiwa bado umeajiriwa. Ni kitabu ambacho kila mwajiriwa anapaswa kukisoma kwa sababu kina maarifa muhimu ya kumwezesha mwajiriwa kujikomboa kiuchumi.
Kila mmoja wetu anajionea wazi jinsi ambavyo hali ya ajira imebadilika na kuzidi kubadilika kadiri siku zinavyokwenda. Upatikanaji wa ajira umekuwa wa shida sana, wenye sifa ni wengi lakini nafasi za ajira ni chache. Na hata wale wanaobahatika kupata ajira, kipato kutoka kwenye ajira hizo ni kidogo sana kiasi kwamba ni vigumu mtu kuweza kuendesha maisha yake vizuri.
Hata zile njia ambazo watu walikuwa wanatumia kujipatia kipato cha ziada kwenye ajira kama posho, marupurupu na hata rushwa kwa sasa vimedhibitiwa kwa kiasi kikubwa. Hivyo njia pekee kwa waajiriwa kuweza kuongeza kipato chao na kujitengenezea uhuru wa kifedha ni kuwa na vyanzo mbadala vya mapato.
Kupitia kitabu hiki cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, unakwenda kupata mwongozo sahihi utakaokuwezesha wewe kuwa na vyanzo mbadala vya kipato huku ukiendelea na ajira yako. Utajifunza jinsi ya kuanzisha biashara na kuikuza bila ya kujali unaanzia wapi. Utajifunza aina mbalimbali za biashara unazoweza kufanya ukiwa umeajiriwa. Pia utajifunza uwekezaji unaoweza kuanza kufanya ukiwa hapo kwenye ajira yako.
Kikubwa na muhimu zaidi utajifunza mifereji nane ya kipato unayotakiwa kujijengea ili kuweza kufikia uhuru wa kifedha. Kwa sababu mfereji mmoja ulionao sasa ambao ni mshahara, hauwezi kukufikisha kwenye uhuru wa kifedha. Utajifunza changamoto na hatari za kuepuka na pia kuweza kuilinda kazi yako pale unapofanya biashara.
Toleo la kwanza la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA lilitoka mwezi Oktoba 2016. Tangu wakati huo mpaka sasa, watu wengi wamenufaika sana na maarifa yaliyopo kwenye kitabu hiki. Wengi wameweza kuanzisha biashara zao wakiwa kwenye ajira na wapo ambao biashara hizo zimewawezesha kuacha ajira zao na kwenda kusimamia biashara zao kikamilifu.
Kwenye toleo hili la pili tutapata shuhuda za wale waliosoma toleo la kwanza na kuchukua hatua, watatuonesha maisha waliyokuwa nayo kabla ya kusoma kitabu, waliyojifunza kwenye kitabu, hatua walizochukua, mafanikio waliyopata na changamoto walizokutana nazo. Lakini pia watakuwa na ushauri kwa wale ambao bado wameajiriwa na hawana kipato chochote cha ziada tofauti na mshahara.
Toleo la kwanza lilikuwa na sura 20, lakini toleo hili linakuja na sura kumi, ila hakuna kilichopunguzwa kutoka kwenye toleo la kwanza. Sura zimepangiliwa vizuri ili kuleta urahisi wa kusoma na hata kurejea wakati mtu unapokuwa umeingia kwenye biashara.
Toleo hili la pili litakuwa na maarifa mapya ambayo hayakuwepo kwenye toleo la kwanza. Maarifa hayo ni jinsi ya kutengeneza mfumo bora wa kuendesha biashara yako ambao utakupa uhuru. Kwa sababu wengi wanaotoka kwenye ajira na kwenda kufanya biashara, wanaishia kutegemewa na biashara zao kiasi kwamba wanakosa uhuru walioufuata kwenye biashara.
Pia kwenye toleo hili la pili kuna michanganuo ya biashara kumi na mbili ambazo unaweza kuanza kuzifanya ukiwa kwenye ajira. Michanganuo hiyo inakupa mwanga wa jinsi unavyoweza kupangilia wazo lolote la biashara ulilonalo na kuweza kuanzia pale ulipo sasa. Michanganuo hiyo ni kutokana na uzoefu wa wale ambao wanafanya biashara hizi, hivyo unakwenda kujifunza moja kwa moja kutoka kwa wafanyaji wa biashara zilizochanganuliwa.
Toleo hili la pili la kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA ni mwongozo sahihi kwa kila mtu aliyeajiriwa na anayetaka kuwa na uhuru wa kifedha anapaswa kuutumia. Kwani tuna mifano ya watu wengi ambao wamejaribu biashara wakiwa kwenye ajira na kuishia kushindwa na kupata hasara kubwa. Hiyo yote inatokana na kukosa maarifa na mwongozo sahihi. Kwa kusoma kitabu hiki, unakwenda kupata mwongozo huo na kuepuka makosa yanayowafanya wengi kushindwa.
Rafiki yangu mpendwa (wasomaji wote wa kazi zangu ni marafiki zangu, hivyo tangu sasa wewe ni rafiki yangu), soma kitabu hiki kwa kina, na usiishie tu kukisoma na kufurahia bali chukua hatua kwa kuyaweka mafunzo haya unayoyapata kwenye matendo ili uweze kutoka hapo ulipo sasa na kupiga hatua zaidi.
Nakutakia kila la kheri kwenye usomaji wa kitabu hiki, nina imani utajifunza mengi na utayatumia kwenye kazi yako, biashara yako na maisha yako kwa ujumla. Na kwa kuwa umeshakuwa rafiki yangu, basi usisite kunitafuta wakati wowote kama utahitaji ushauri au mwongozo zaidi kwenye hatua unazochukua kwenye kuanzisha biashara yako. Nina huduma mbalimbali za ushauri na ukocha ambazo zitakuwezesha kupiga hatua zaidi. Kupata maelezo ya huduma za ukocha, soma mwisho wa kitabu hiki kwenye kipengele cha bidhaa na huduma za kocha.
Naamini kitabu hiki kinakwenda kuwa mwanga mpya kwenye maisha yako, kama utachukua hatua kwenye yale utakazojifunza.
Chukua hatua sasa ya kupata kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA, kwa kuwasiliana na namba 0678 977 007.
Kwenye kipindi cha ONGEA NA KOCHA hapo chini nimekupa ufafanuzi zaidi kuhusu kitabu cha BIASHARA NDANI YA AJIRA. Karibu ujifunze na kuweza kuchukua hatua.
Nenda kayaweke haya uliyojifunza kwenye matendo ili uweze kujenga mafanikio makubwa kwenye maisha yako kwa kuiishi kila siku yako kwa mafanikio makubwa.
Kutoka kwa rafiki yako anayekupenda na kukujali sana,
Kocha Dr. Makirita Amani,
Daktari |Mwandishi |Kocha |Mkufunzi
+255 678 977 007 / amakirita@gmail.com
MUHIMU; Rafiki, nikushukuru kwa kuendelea pamoja kupitia mafunzo haya ninayotoa. Karibu kwenye huduma zaidi ninazotoa, kuanzia 1. VITABU, 2. NGUVU YA BUKU, 3. KISIMA CHA MAARIFA, 4. CHUO CHA MAUZO na 5. BILIONEA MAFUNZONI. Kupata maelezo ya huduma hizi, tumia mawasiliano yaliyopo hapo juu. Karibu sana.